Siku kama ya leo Oktoba 19 mwaka wa 1996 alizaliwa staa wa muziki wa Hiphop na mwaandishi wa nyimbo kutoka nchini Marekani Lil Durk.
Jina lake halisi ni Durk Derrick na alizaliwa huko Chicago Illinois nchini Marekani ambako alianza muziki mwaka wa 2009 lakini alikuja akapataa umaarufu mwaka wa 2011 baada ya kuachia ngoma zake mbili ambazo ni Sneak Dissin na Ima Hitta zilizopokelewa kwa ukubwa nchini Marekani.
Mwaka wa 2012 Lil Durk aliachia mixtape yake inayokwenda kwa jina la Life Aaint No Joke chini ya lebo ya muziki ya OTF ikafuatwa na mixtape yake iitwayo Signed To The Street ya mwaka wa 2013 ambayo ilitayarishwa na lebo ya muziki ya Def Jam Recordings.
Mwaka wa 2014 Lil Durk aliachia mixtape nyingine iitwayo The Sequel to Signed to the Streets ikafuatwa na album yake ya kwanza ya mwaka wa 2015 iitwayo Remember My Name, album ambayo ilikuwa na jumla ya ngoma 10 za moto.
Mwaka huo huo wa 2015 Lil Durk aliachia mixtape yake inayokwenda kwa jina la 300 days, 300 Nights ambayo ilikuwa ngoma kama My Beyonce ambayo iliweza kufikia viwango vya mauzo ya gold kwa kuuza zaidi ya nakala laki 5.
Mwaka wa 2016 Lil Durk aliachia album yake ya pili iitwayo Lil Durk 2X ambayo ilikuwa na jumla ya ngoma 11 akiwa amewashirikisha wasaani kama young thug,ty dolla sign na wengine kibao.
Hata hivyo tangu Lil Durk aanze kujishughulisha na muziki wa hiphop nchini Marekani mwaka wa 2009 amefanikiwa kufanya jumla ya album tano za muziki,Mixtape 12,Singles 20 na album mbili iliyobeba nyimbo zilitoka pamoja na zile hazikutoka.
Lil Durk kwa sasa amesainiwa na lebo ya muziki ya Def Jam Records lakini pia yupo chini ya record lebo ya Coke Boys inayomilikiwa na rapa French Montana ambayo inafanya kazi pamoja na lebo yake ya muziki ya Only the Family.