You are currently viewing LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 21, ALIZALIWA MWANASOKA WA ZAMANI WA MANCHESTER UNITED NEMANJA VIDIC

LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 21, ALIZALIWA MWANASOKA WA ZAMANI WA MANCHESTER UNITED NEMANJA VIDIC

Siku kama ya leo Oktoba 21 mwaka wa 1981 alizaliwa mwanasoka wa zamani wa Serbia na klabu ya Manchester United, Nemanja Vidic.

Vidic alizaliwa huko titovo Yugoslavia ambako alianza soka katika klabu ya Red Star Belgrade  mapema miaka ya 2000 kabla ya kujiunga  ya Sparta Moscow ya nchini Urusi mwaka wa 2004.

Akiwa Sparta Moscow Namanja Vidic  alifanikiwa kuichezea klabu ya hiyo mechi 39 huku akitia kimiani magoli manne  kwa misimu miwili aliyoichezea klabu hiyo.

Mwaka wa 2006 alitimukia nchini England na kuidaka saini ya klabu ya Manchester United kwa pauni millioni 7 ambapo aliisaidia klabu hiyo kutwaa mataji matano ya Premier,taji la klabu Bingwa Barani Ulaya, Kombe la Fifa na makombe 6 ya Ngao ya Jamii.

Akiwa Manchester, Vidic alifanikiwa kuichezea klabu hiyo mechi 211 huku akifunga magoli 15 kwa misimu minane aliyoitumikia klabu ya Manchester United.

Baada ya kutumikia klabu ys Manchester United kwa miaka minane Vidic alijiunga na klabu ya Inter Milan inayoshiriki ligi kuu nchini Italia kwa uhamisho wa bure lakini baada kuichezea klabu hiyo mechi 23 na kufanga goli moja, Namanja Vidic alitangaza kustaafu soka ya kimataifa mwaka wa 2016.

Katika ngazi ya kitaifa, Namanja Vidic ameichezea timu ya taifa ya Serbia katika ngazi ya vijana na watu wazima ambapo amewaikilisha taifa lake kwenye michuano ya Euro mwaka wa 2004 na kombe la dunia mwaka wa 2006 huku akichezea mechi  56 na kufunga magoli mawili tangu mwaka wa 2002.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke