Siku kama leo Oktoba 22 mwaka wa 1968 alizaliwa mkali wa Miondoko ya Regge na Dancehall, ambaye pia ni Muigizaji na DJ kutoka Nchini Jamaica, Shaggy.
Jina lake halisi ni orville Richard Burell na alizaliwa huko Kingston, nchini Jamaica ambako alianza muziki mwaka wa 1993 alipoachia album yake wa kwanza iitwao “Pure Pleasure” ikafuatwa na Original Doberman ya mwaka 1994,Boombastic ya mwaka wa 1996 na Midnite Love ya mwaka wa 1997.
Mwaka wa 2000 Shaggy aliachia album yake ya tano iitwayo “HOT SHOT”,album ambayo ilifanikiwa kufika viwango vya mauzo ya Platnumz Mara Sita nchini Marekani lakini pia ilishika namba moja kwenye chati ya Billboard Hot 200 japo album zake zilizofuata za Lucky Day ya mwaka wa 2002 na Clothes Drop zilishindwa kufikia mafanikio ya Album ya Hotshot.
Hata hivyo tangu aanze muziki mwaka wa 1993 Shaggy ameshafanya jumla ya 12 za muziki, Singles 88 na album 7 za nyimbo zilizotoka pamoja na zile hazikutoka.
Kutokana na mafanikio aliyoyapata kwenye muziki wake, Shaggy ameteuliwa kuwania kwenye tuzo mbali mbali na ameshinda tuzo mbili za Grammy kupitia album yake ya Boombastic ya mwaka wa 1996 na 44/876.
Kando na muzik,i Shaggy amewahi kuwa mwanajeshi wa majini nchini Marekani kabla hajeanza muziki lakini pia ni muigizaji kwani ameigiza kwenye filamu nyingi nchini Marekani ikiwemo Blast ya mwaka wa 2004 Game Over Man ya mwaka wa 2018, American Idol ya mwaka wa 2019 na nyingine kibao.
Shaggy anakadiriwa kuwa na utajiri wa Dolla Milioni 12, mafanikio ambayo aliyapata zaidi kupitia albums za BOOMBASTIC na HOTSHOT.