You are currently viewing LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 23,ALIZALIWA STAA WA MUZIKI WA RNB KUTOKA MAREKANI, MIGUEL.

LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 23,ALIZALIWA STAA WA MUZIKI WA RNB KUTOKA MAREKANI, MIGUEL.

Siku kama ya leo Oktoba 23 mwaka wa 1983 alizaliwa Staa wa muziki wa RnB kutoka Marekani Miguel.

Jina lake halisi ni Miguel Jontel Pimentel na alizaliwa huko San Pedro, Carlifonia nchini Marekani ambako alianza muziki akiwa na umri wa miaka 13 lakini alikuja kupata umaarufu zaidi nchini Marekani mwaka wa 2010 alipoachia album yake ya kwanza iitwayo “All I Want isYou” chini ya lebo ya muziki ya Jive Records

Baada ya lebo ya muziki ya Jive Records kuvunjwa,miguel alisaini mkataba wa kufanya kazi na lebo ya muziki ya RCA Records ambayo ilisimamia shughuli zote za album yake ya pili iitwayo Kaleidoscope Dream ya mwaka wa 2012.

Mwaka wa 2015 Miguel aliachia album yake ya tatu iitwayo Wildheart ikafuatwa na album yake ya nne inayokwenda kwa jina la “War & Leisure” ya mwaka wa 2017. Hata hivyo tangu aanze muziki miguel ameshafanya jumla ya album nne za muziki,Singles 21,Mixtape nne,na EP nne.

Kutokana na mafanikio yaliyopata kwenye muziki wake, Miguel ameteuliwa kunawania tuzo 41 za muziki nchini Marekani na ameshinda tuzo saba za muziki ikiwemo tuzo moja ya Grammy,tuzo mbili za BET Awards, na tuzo nne za Soul Train Music Awards.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke