You are currently viewing LEVIXONE AOMBA MASHABIKI WAMCHANGIA KWA AJILI YA KUWASAIDIA MAYATIMA

LEVIXONE AOMBA MASHABIKI WAMCHANGIA KWA AJILI YA KUWASAIDIA MAYATIMA

Kwa kawaida, kwenye kila sherehe au matatizo, suala la michango huwa ni kigugumizi kikubwa kwa watu wengi duniani

Hii imekua tofauti kidogo kwa Msanii wa Nyimbo za Injili kutoka nchini Uganda Levixone ambaye amekuja na mbinu tofauti ya kupata zawadi kutoka kwa marafiki zake kwenye siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

Levixone ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa Desemba 7 mwaka huu, ametumia ukurasa wake wa instagram kuwataka mashabiki kumchangia pesa kwenye kampeni yake ambayo ameanzisha kwa ajili ya kutoa msaada kwa watoto wenye uhitaji katika jamii yake.

Levixone ambaye anatokea katika vitongoji duni vya Kosovo nchini Uganda, amekuwa akifanya jitihada za kuwasaidia watoto wanaotoka mitaa ya mabanda tangu alipopenya kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda miaka michache iliyopita.

Ikumbukwe wiki chache zilizopita, msanii Pallaso pia aliwaomba mashbiki wamchangia kiasi cha shillingi millioni 5.2 ili kuitoa gari lake la aina ya Range Rover iliyokuwa imeshikiliwa na mamlaka ya kukusanya ushuru nchini Uganda  URA.

Hata hivyo hitmaker huyo “Malamu” hakufikia lengo  hilo, hivyo akatoa pesa zilizokusanywa kwa watu wenye uhitaji katika jamii.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke