Wasanii kutoka marekani Chris Brown na Lil Baby wametangaza kuja na ziara ya pamoja ambayo wameipa jina la “One Of Them Ones”.
Ziara hiyo itapita kwenye miji 27 nchini Marekani na imepangwa kuanza Julai 15 na kumalizika Agosti 27 mwaka huu.
Kwa upande wa Chris Brown, ziara hii inakuja huku kukiwa na tetesi za ujio wa Album yake mpya iitwayo “Breezy” ambapo tayari ameachia mkwaju mmoja uitao ‘WE (Warm Embrace)’ na hajafanya ziara tangu mwaka 2019 alipofanya Indigo Tour.
Kwa Lil Baby vile vile naye anatarajiwa kuachia Album mpya kwani tayari amedondosha ngoma mbili; ambazo ni “Right On” na “In a Minute.”