You are currently viewing LIL DUVAL APINGA BLAC CHYNA KUINGIZA KSHS. BILLIONI 2.4 KUPITIA ONLYFANS

LIL DUVAL APINGA BLAC CHYNA KUINGIZA KSHS. BILLIONI 2.4 KUPITIA ONLYFANS

Mchekeshaji na Muigizaji Lil Duval ameibuka na kuzungumzia ishu ya Blac Chyna kutengeneza zaidi ya KSh. Bilioni 2.4 kila mwezi mwaka 2021 kwenye mtandao wa OnlyFans.

Kupitia mfululizo wa post zake kwenye mitandao ya kijamii, Mchekeshaji huyo amesema huu ni uzushi mtupu na hakuna ukweli wowote. “Siamini kama nyie wote mnaamini Blac Chyna alitengeneza kiasi hicho cha pesa ($20 million) kwa mwezi kupitia OnlyFans. Hapa ndio nafahamu sasa ninyi nyote hamuishi kwenye uhalisia.” aliandika Lil Duval na kucheka kisha kuongeza

“Mnaamini kila mnachokiona kwenye vichwa vya habari, na hata hamuulizi. Nimeona Wanawake waki-post na kusema ‘Naweza kuamini’ hii ni ushahidi kwamba nyie wote hamjui ($20 Million) ilivyo. Mmiliki wa OnlyFans ameanika hilo ili kuwapumbaza vichwa vyenu na mfungue akaunti zenu. Namba hazidanganyi, lakini kwa hili wametupanga.” alimalizia Lil Duval.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke