You are currently viewing Lil Wayne ashtakiwa na mpishi wake

Lil Wayne ashtakiwa na mpishi wake

Rapa Lil Wayne ameshtakiwa na mpishi wake wa zamani ambaye amedai kwamba alifukuzwa kazi kimakosa kwasababu alienda kumuuguza mwanae mwenye umri wa miaka 10.Kwa mujibu wa Blast mpishi huyo Morgan Medlock  anasema kwamba alifukuzwa kazi baada ya kuondoka pale alipogundua kuwa mtoto wake amepata majeraha ya kichwa

Morgan ambaye kwa wakati huo alikuwa mjini Las Vegas pamoja na Wayne, ameeleza kwenye nyaraka zake za mahakama kwamba alitaka kurudi Los Angeles akakae na mtoto wake lakini ndege ilikuwa imechelewa kuondoka kwasababu wayne alikuwa busy sana akivuta ndani ya ndege na hivyo kuamua kuchukua ndege nyingine na kuambiwa atoe taarifa pale atakapokuwa na mwanae

Alipoulizwa kama ataachana na kazi hiyo Morgan alisema hapana hana nia ya kuacha kazi kwa muda huo ambapo alijibu kwa njia ya meseji “No” baada ya muda mfupi alishangaa amejibiwa “goodbye” “Tell Morgan this isn’t going to work” . Jibu la Lil Wayne kwa msaidizi wake akitaka amwambie mpishi huyo kuwa hawataendelea nae kikazi

Morghan alishangazwa kabisa na kuvunjwa kwa mkataba wake ghafla, na hivyo aliamua kufungua kesi akidai fidia zaidi ya Ksh.Milioni 56.8

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke