Rapa Lil Wayne ametangaza ujio wa awamu ya sita wa tamasha lake la “Lil WeezyAna Festival” huko New Orleans nchini Marekani.
Tamasha hilo ambalo mwaka 2019 ndio ilikuwa mara yake ya mwisho kufanyika baada ya katazo la mikusanyiko kutokana na janga la Corona, sasa linarudi kivingine mwaka huu na litafanyika Agosti, 27 katika eneo la Champion’s Square.
Kikubwa ambacho Lil Wayne anajivunia kutokana na tamasha hilo ni kwamba sehemu ya pesa ambazo zitakusanywa kutokana na mauzo ya tiketi zitatumika kufadhili elimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya eneo hilo la New Orleans Louisiana ambalo ni nyumbani kwao.
Rais wa kampuni ya muziki ya Lil Wayne iitwayo Young Money Records, Mack Maine ambaye pia ni rappa, kwenye mahojiano na COMPLEX amesema atatumia fursa ya tamasha hilo kutoa heshima kwa waliopoteza maisha kwenye kimbunga cha Katrina miaka 17 iliyopita.
Lakini pia amesema kwenye msimu huu wa sita wa tamasha hilo kutahudhuriwa pia na wageni maalumu.