Mkali wa muziki wa hiphop kutoka marekani Lil Wayne anatarajiwa kutumbuiza nchini Uingereza kwa mara ya kwanza baada ya miaka 14.
Rapa huyo atatumbuiza nchini humo mwezi Juni mwaka huu katika tamasha la Strawberries & Creem.
Mwaka 2011 hati ya usafiri ya Lil Wayne ilisitishwa na Serikali ya Uingereza kufuatia kukutwa na hatia ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.