Mke wa Juliani, Lilian Ng’ang’a ameshindwa kuwavumilia watu wanaozidi kumkejeli mtandaoni kwa hatua ya kuingia kwenye ndoa na mwimbaji huyo.
Kilichomuumiza zaidi mrembo huyo ni kitendo cha watu kuhoji kuwa ilikuwa ni fedhea kwake kuacha utajiri wa Alfred Mutua na kisha kukimbilia maisha ya taabu kwa Juliani.
Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Ng”ang’a ameonekana kukerwa na watu wanaomsema vibaya mtandaoni kwa kuandika ujumbe uliotafsiri kuwa hajutii kumuacha Mutua na kumpenda Juliani ambaye ni mwanamuziki.
Lilian ambaye amejaliwa kupata mtoto na Juliani amesema hana muda kabisa wa kupishana na walimwengu ambao hawana shughuli ya kufanya mtandaoni huku akiwataka waendelea kumsema vibaya kwani hana uwezo wa kuthibiti kile wanachomuwazia.
Kauli ya Lilian Ng’ang’a inakuja mara baada ya watu kulinganisha utajiri wa mpenzi wake wa sasa Juliani na mume wake wa zamani Alfred Mutua ambaye kwa wakati mmoja aliwahi kuwa gavana wa kaunti ya Machakos.