You are currently viewing LINEX AMCHANA BABA LEVO KWA MADAI YA KUMZUNGUMZIA VIBAYA

LINEX AMCHANA BABA LEVO KWA MADAI YA KUMZUNGUMZIA VIBAYA

Mwanamuziki wa Bongofleva Linex mjeda ameamua kumtolea uvivu baba levo baada ya msanii huyo kuendelea kuongelea maisha yake mara kwa mara kwenye vyombo vya habari

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Linex amemchana Baba Levo kuwa aache kuongelea maisha yake kwenye redio kwani jambo hilo linamkosesha amani huku akimuomba baba levo msamaha kama amewahi kumkosoa.

Linex na Baba Levo ni marafiki wa miaka mingi na Baba Levo ameshawahi kukiri mara nyingi kuwa Linex ni kati ya watu ambao walimsaidia miaka ya hapo nyuma akiwa Dareesalaam akijaribu kuupambania kipaji chake cha muziki.

Hata hivyo Baba Levo amekuwa akifunguka matukio na tabia za Linex ambazo walikuwa wanazipitia miaka ya nyuma. Lakini pia amekuwa akilitaja jina la Linex kwenye mifano mbalimbali afanyapo mahojiano na vyombo vya habari jambo ambalo limemfanya Linex kukwazika

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke