Nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Linex Mjeda yupo mbioni kuachia EP yake mpya ya nyimbo za Dini, ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo tofauti na alivyozoeleka akiimba nyimbo za kidunia.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Linex amezungumzia ujio wa EP yake, kwa kusema kwamba alikuwa na ndoto ya kutoa kazi yenye nyimbo za dini, hivyo amefurahi kuona ametimiza ndoto yake hiyo.
EP ambayo ameipa jina la ‘MY SIDE B’ ina jumla ya ngoma 4, ambazo ni “Umepotea”, “Mtetezi”, “Utaniona” na “Tusafishe”.
Katika upande wa Bongo Fleva msanii Linex hivi karibuni aliachia ngoma yake iitwayo “Sawa Baby” akiwa amemshirikisha Pallaso ambayo pia imefanikiwa kufanya vizuri katika mtandao wa Youtube.