You are currently viewing LINEX SUNDAY MJEDA AACHIA EP YAKE MPYA

LINEX SUNDAY MJEDA AACHIA EP YAKE MPYA

Msanii wa Bongofleva Linex Sunday Mjeda ameachia rasmi EP yake mpya ya nyimbo za Dini, ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo tofauti na alivyozoeleka akiimba nyimbo za kidunia.

EP hiyo ambayo ameipa jina la My Side B ina jumla ya nyimbo 4 za moto ambazo amezifanya bila kumshirikisha msanii yeyote.

EP hiyo ina nyimbo kama “Umepotea”, “Mtetezi”, “Utaniona” na “Tusafishe” na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mtandao wa kukisikiliza na kupakua muziki wa Boomplay.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Linex amesema kwamba alikuwa na ndoto ya kutoa kazi yenye nyimbo za dini, hivyo amefurahi kuona ametimiza ndoto yake hiyo.

My side b ni EP ya tatu kwa mtu mzima Linex tangu aanze safari yake ya muziki  baada ya tatu za mjeda ep ya mwaka wa 2021 na dunia nyingine ya mwaka wa 2020.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke