You are currently viewing LJAY MAASAI AKIRI KUPATWA NA MSONGO WA MAWAZO KIASI CHA KUTAKA KUJIUA

LJAY MAASAI AKIRI KUPATWA NA MSONGO WA MAWAZO KIASI CHA KUTAKA KUJIUA

Mwanamuziki L Jay Maasai ameamua kutoa ushuhuda wa ndani kuhusu maisha yake,amefunguka kwamba aliwahi kutaka kujiua mara tatu.

Kwenye mahojiano na SPM Buzz, msanii huyo  amefunguka mengi kuhusu tatizo la afya ya akili na safari yake ya kupona kwa kusema kwamba aliingia kwenye msongo wa mawazo baada ya watu kumchukulia kuwa ana tajiiri mkubwa aliposhinda tuzo ya msanii bora wa kiume mwaka 2016 kwenye tuuzo za Groove Awards.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Laleiyo” amesema kitendo hicho kilimfanya kuingiwa na hofu kiasi cha kuanza kujitenga na watu kwani aliogopa sana kuombwa pesa.

Msanii huyo ameenda mbali zadi na kusema kwamba aliamua kuacha kila kitu na kujifirikia kwanza kama njia ya kujitibu lakini kilichomsaidia zaidi ni kitendo chake cha kufunguka kilichokuwa kinamsibu kupitia mitandao yake ya kijamii licha ya watu kumbeza.

Hata hivyo amesema kwa sasa hali yake imerejea katika hali yake ya kawaida huku akiwahimiza watu ambao wanapitia msongo wa mawazo maishani wajitokeze na wazungumzie hali zao kwa ajili ya kupata usaidizi kwani wakichukulie poa suala hilo wataathirika kiakili.

Kwa sasa Ljay Maasai yupo kwenye uongozi mpya uitwao STM anajianda kuachia ngoma mfululizo bila kupoa licha ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke