Mwanamuziki Lydia Jazmine Jazmine amedai kuwa kuna mgawanyiko mkubwa katika biashara ya muziki, haswa miongoni mwa wasanii wa kike nchini Uganda.
Akizungumza kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Nina Roz, Jazmine amesema wasanii wakike wamekuwa wakionea wivu kimya hasa mmoja wao anapofanya vizuri kimuziki ambapo ameenda mbali na kudai muziki una nafasi kubwa ambayo inawatosha wasanii wote hivyo haoni umuhimu wa wasanii kutakiana mabaya.
Msanii huyo amewataka wasanii wa kike nchini Uganda kuacha kutengeneza mazingira ya kugombana na badala yake washirikiane kwenye suala la kuipeleka mbele tasnia ya muziki nchini humo kimataifa.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “I Love you Bae” amesema atakuwa anahudhuria shughuli ya wasanii ambao ni wakweli huku akisusia ya watu ambao amewataja kama wanafiki
Hata hivyo watu wengi wamehoji kuwa alikuwa anamrushia vijembe Spice Diana kwa kuwa hakuhudhuria hafla ya usikilizwaji wa albamu yake.