Rapa kutoka Marekani Lil Wayne amefikia rekodi ya mauzo ya Diamond ambayo ameinasa kupitia single yake “Lollipop” iliyotoka mwaka 2008.
“Lollipop” ambayo Lil Wayne alimshirikisha Static Major ambaye alifariki wiki mbili kabla ya kuachiwa kwa wimbo huo, unakuwa wimbo wa kwanza kwa mtu mzima Wayne kufikia mauzo hayo.
Sanjari na hilo, wimbo huo ndio wimbo wenye mafanikio zaidi katika maisha ya muziki ya Lil wayne ambapo ulitajwa kuifanya album yake ya “Tha Careter III” kuuza zaidi ya Units Million Moja katika wiki yake ya kwanza na kunyakua tuzo ya Grammy mwaka 2009 kama Best Rap Song.