You are currently viewing LOUI AWEKA REKODI BILLBOARD AFRIKA KUSINI

LOUI AWEKA REKODI BILLBOARD AFRIKA KUSINI

Msanii wa Bongofleva Loui anaendelea kufanya makubwa kupitia  chati kubwa za Billboard Afrika Kusini.

Hitmaker huyo wa “Hennessy”  amefikia hatua hiyo baada ya wimbo wao na mwimbaji Musa Keys kutoka Afrika Kusini,  uitwao “Selema (Po Po)” kuendelea kusalia kwenye chati hiyo ukiwa nafasi ya 20 kwa nyimbo zinazofanya vizuri Afrika Kusini, wiki hii.

Kwa mujibu wa chart data tz wimbo huo umekaa kwenye chart hizo za Billboard kwa jumla ya wiki 13 na ulifanikiwa kushika nafasi za juu.

Utakumbuka, wimbo huo wa “Selema” pia umeshafikia kiwango cha mauzo ya PLATNUM kwa Afrika Kusini, hivyo unamfanya msanii Loui kuwa miongoni mwa wasanii wa Tanzania kufikia mafanikio hayo baada ya msanii Diamond Platnumz.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke