Msanii wa Bongofleva, Lulu Diva kwa mara ya kwanza kabisa amefunguka kuhusu sakata la kuvujishwa kwa video zake za faragha kwenye mitandao ya kijamii.
Lulu Diva amesema kwamba video hiyo ilivujishwa na aliyekuwa mwanaume wake ambaye kwa sasa anaishi nchini Uingereza.
“Nilikuwa naongea naye kimapenzi kama mpenzi wangu, ni mtu ambaye nilikuwa huru naye kwa sababu niliona ni kama mtu mzima,” amesema na kuendelea.
“Kama sasa hivi nimebaki kujiuguza, lakini kama mwanaume ambaye nilikuwa naongea naye kama mpenzi wangu, unajua unaweza ukawa huru naye na kujiachia kama umetoka kuoga, ukawa uko wapi, hivo. Hata sijui hizo video anazo ngapi. Sijajirekodi mimi, amenirekodi yeye,” alisema Lulu Diva.