Nyota wa Filamu nchini Lupita Nyongo ameweka wazi kuwa anachumbiana na mpenzi wake ambaye ni ripota wa michezo na muasisi mwenza wa kampuni ya mavazi ya Surfapparel Company ,Selema Masekela.
Lupita amethibitisha habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuposti video hii na kisha akaambatanisha na maneno yanayosomeka, “We just click! @selema #thisismylove #nuffsaid”
Hata hivyo mashabiki na mastaa mbali mbali wamempongezwa kwa hatua hiyo kubwa maishani huku wakiwataka kila la kheri katika safari yao mpya ya mapenzi.
Utakumbuka Lupita Nyongo hajakuwa na mazoea ya kuanika mambo yake ya mahusiano mtandaoni ila kumekuwa na tetesi kuwa huenda mrembo huyo aliwahi kuwa penzni na mwigizaji wa filamu maarufu ya “Black Panther” Chadwick Boseman aliyefariki Agosti 28 mwaka 2020 kutokana na saratani ya utumbo.