Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Lydia Jazmine amesema kuwa kuna baadhi ya watu kwenye tasnia ya muziki nchini humo hawatambui mchango wake.
Hitmaker huyo wa “I Love Bae” amesema licha ya kuachia ngoma kali mwaka wa 2021 hajapewa heshima anayostahili kama wasanii wengine wakike nchini uganda.
Mimi ni mmoja wa msanii ambao mwaka huu nimeachia ngoma 4 kali. Baadhi ya watu haoni na kutambua juhudi zangu lakini licha ya haayo yote upendi wenu mashabiki zangu ndio inanipa moyo wa kuendelea kufanya kazi.. Aliandika kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Hata hivyo hajabainika ni kitu gani kilipelekea mrembo huyo kutoa kauli hiyo ila wajuzi mambo kwenye mitandao ya kijamii wanahoji huenda hajafurahishwa na jinsi wasanii wapya wa kike nchini Uganda wanapokea upendo kuliko waliowatangulia.
Ikumbukwe Lydia Jazmine hakushinda tuzo yeyote mwaka wa 2021 nchini Uganda licha ya kuachia ngoma kali kama Banange, Feeling, Kapeesa na nyingine nyingi.