Ni takribani miezi tano imepita kutoka staa wa muziki nchini uganda Lydia Jazmine aachie wimbo wake uitwao “Kapeesa”
Ukimya wa Lydia Jazmine kwenye muziki umekuwa na maswali mengi sana kwa mashabiki na wadau wa muziki nchini Uganda.
Sasa kwenye mahojiano yake hivi karibuni Lydia Jazmine ameweka wazi sababu zilizofanya akae kimya kwa miezi hiyo yote huku utaratibu wake wa kuachia nyimbo kwa miaka miwili ukiwa wa kusuasua.
Lydia Jazmine ameweka wazi kuwa alikuwa anasumbuliwa na tatizo la vidonda vya tumbo ulcers kwa zaidi ya miezi tano ila kwa sasa anamshukuru mungu amepona.
Mrembo huyo ameweka wazi hilo alipokuwa anatambulisha wimbo wake mpya uitwao “Tonkoseza” ambapo amewataka mashabiki zake kukaa mkao kupokea nyimbo zake ambazo atakuwa anaachia back to back.