Kwa miaka mingi sasa msanii Lydia Jazmine amekuwa akihisishwa kutoka kimapenzi na Eddy Kenzo.
Wakati Eddy Kenzo aliachana na baby mama wake Rema Namakula mashabiki walimtuhumu kwamba yeye ndiye chanzo cha ndoa ya Bosi huyo wa Lebo ya muziki ya Big Talent kuingiwa na ukungu.
Sasa akiwa kwenye moja ya Interview Lydia Jazmine amedokeza kwamba anafahamu kuwa mashabiki wanadhani kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Eddy Kenzo jambo ambalo anadai sio kweli.
Hitmaker huyo wa “I Love You Bae” ameenda mbali zaidi na kutoa ya moyoni kwa kusema kwamba yuko tayari kuolewa na Eddy Kenzo iwapo atatia nia ya kumchumbia kwa sababu ni moja kati ya watu ambao wana uelewa mpana kwenye masuala ya muziki.