You are currently viewing MAANDY AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA BREEDER LW.

MAANDY AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA BREEDER LW.

Msanii wa muziki nchini Maandy amekanusha kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na rapa Breeder Lw.

Akiwa kwenye moja ya interview Maandy amesema haoni shida yeyote rapa huyo akimzimia kimahusiano ila hawezi chumbiana naye kwani mitindo yao ya maishi ni tofauti.

Hata hivyo hitmaker huyo wa Sirudi Home amewataka mashabiki kutofuatilia sana maisha yake ya mahusiano na badala yake waelekeze nguvu zao kwenye muziki wake.

Kauli ya mrembo huyo imekuja mara baada ya watu kumhusisha kuwa anatoka kimapenzi na breeder lw kutokana na collabo nyingi ambazo wamezifanya kwa pamoja.

Maandy alianza muziki mwaka wa 2016 chini ya lebo ya muziki ya Chuo records ambapo ameenda mbali zaidi na kuachia hits kama Pon  It, Shash na nyingine kibao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke