Female rapper kutoka Kenya, Maandy amepuzilia mbali uvumi wa muda mrefu kuwa anatoka kimapenzi na Mejja.
Akipiga stori na Podcast ya Nicholas Kioko kwenye mtandao wa youtube, Maandy amekanusha madai hayo kwa kusema kwamba uhusiano wake na msanii huyo ni wa kirafiki tu na kwa sasa anafurahia maisha yake akiwa hana mpenzi yaani single!
Hitmaker huyo ngoma ya “By The Way” amesema licha ya kusumbuliwa na wanaume wengi, kwa sasa hataki kukurupuka kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi kutokana na yeye kujikita zaidi katika muziki wake.
Uvumi wa Maandy kutoka kimapenzi na Mejja ulianza miezi kadhaa iliyopita baada ya wawili hao kuonekana wakiwa pamoja studio waki-vibe na mdundo wa singo yao mpya.
Kwa sasa Maandy anafanya vizuri na wimbo wake uitwao Ka Unaweza aliomshirikisha Mejja, wimbo ambao una zaidi ya Views laki 2 youtube ndani kipindi cha siku 2 tangu kuachiwa kwake.