You are currently viewing MAANDY AWAJIBU WANAODAI ANATOKA KIMAPENZI NA MAPRODYUZA

MAANDY AWAJIBU WANAODAI ANATOKA KIMAPENZI NA MAPRODYUZA

Msanii wa kike nchini Maandy amewajibu wanaodai kuwa mafanikio yake kimuziki yametokana na yeye kutoka kimapenzi na maprodyuza wa muziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram hitmaker huyo wa ngoma ya “By The Way” ameonakana kukasirishwa na wanaomema vibaya kwa kusema kwamba tuhuma hizo hazina ukweli wowote bali zimeibuliwa na watesi wake ambao wanalenga kumuharibia jina.

Mrembo huyo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba kama kweli  angekuwa anajiuza kimwili kwa maprodyuza angeshapeleka muziki wake kimataifa kitambo.

“Huko clock app Wanasema Nagawa mbaya . If I was to use my body to get ahead , ningekua Grammies nikipigania space na Beyoncé ,si hapa ungwaro 😮‍💨😮‍💨 To the producers I’ve worked with kindly mark register hapa tuone mko wangapi 😂😂😂😂”, Aliandika Instagram.

Hii si mara ya kwanza kwa Maandy kuzushiwa taarifa za aina hii kwani kipindi cha nyuma alidaiwa kutoka kimapenzi na rapa Breeder LW, madai ambayo aliyakanusha vikali.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke