Rapa kutoka Marekani Macklemore anaendelea kuuaminisha umma kwamba hakustahili ushindi kwenye tuzo za Grammy mwaka wa 2014.
Rapa huyo amesema bado anaandika barua za kuomba radhi kwa Kendrick Lamar, Kanye West na Drake kwa ushindi wake wa Tuzo ya Grammy mwa 2014. Macklemore anasema hakuna hata mmoja ambaye amejibu.
Kwenye tuzo za mwaka huo wa 2014, Macklemore aliibuka mshindi wa kipengele cha Best Rap Album kupitia album yake “The Heist” akiwaangusha Drake na album yake “Nothing Was the Same”, Jay-Z “Magna Carta Holy Grail”, Kendrick Lamar “Good Kid, M.A.A.D City” pamoja na Kanye West “Yeezus”