You are currently viewing “MADE IN LAGOS” YAFIKISHA ZAIDI YA STREAMS BILLIONI MOJA

“MADE IN LAGOS” YAFIKISHA ZAIDI YA STREAMS BILLIONI MOJA

Album ya msanii WizKid kutoka Nigeria, “Made in Lagos” Deluxe Edition iliyotoka Agosti 27 mwaka huu yenye hitsong kama Essence Remix, imefanikiwa kufikisha jumla ya streams Bilioni Moja.

Made in Lagos” imefikisha jumla ya streams hizo ikiwa ni mjumuisho wa streams zote za (Deluxe Edition) katika Platform mbalimbali za muziki duniani kama Apple Music (millioni 322.75), Spotify (millioni 229.33), Youtube (millioni 227.82), Audiomack (millioni 178.25), Boomplay (millioni 40.17) na Pandora (millioni 20.1)

WizKid ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani kwenye ziara yake ya kimuziki ya “Made In Lagos Tour”, aliyoianza Septemba 10 mwaka huu, anaendelea pia kufanya vizuri kwa kupata idadi kubwa ya mashabiki kwenye show zake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke