You are currently viewing MADENI YAMUUMBUA RAPA KAA LA MOTO

MADENI YAMUUMBUA RAPA KAA LA MOTO

Rapa Kaa La Moto ameingia kwenye headlines mara ya kukumbwa na tuhuma za kukwepa kulipa deni la shillingi laki 3 analodaiwa na mwanadada aitwaye Lisa Russell

Kwa mujibu wa Lisa Russell Kaa la Moto alimuomba Dola 2,500 atumie kipindi cha corona kwa makubaliano kwamba atamrudishia ila mpaka sasa rapa huyo hajaweza kumlipa deni lake.

Aidha amesema licha ya kumpigia simu ili kumuulizia kuhusu deni hilo,rapa huyo pamoja na meneja wake wameingiwa na jeuri kiasi cha kumtishia maisha, hali inayotoa tafsiri kwamba anataka kumdhulumu.

Mrembo huyo amesema Kaa la Moto afanikiwa kumlipa shilling elfu 58,700 pekee huku akiahapa kutolegeza msimamo hadi pale rapa huyo atakapokamilisha deni lake la sivyo atazidi kuanika maovu yake.

Hata hivyo Kaa la Moto hajajibu tuhuma za kukwepa kulipa deni zilizoibuliwa na Lisa Russell ila ni jambo la kusubiriwa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke