You are currently viewing MADINI CLASSIC AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA MWANAMKE ALIYEMZIDI KIUMRI

MADINI CLASSIC AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA MWANAMKE ALIYEMZIDI KIUMRI

Mwanamuziki Madini Classic amekanusha madai yaliyoibuliwa na walimwengu kuwa analelewa na mwanamke  huko Mombasa.

Katika mahojiano na Nicholas Kioko, Madini amesema madai hayo hayana msingi wowote kwani yameibuliwa na baadhi ya watu ambao wanamwazia mabaya kutokana na mafanikio anayozidi kuyapata kupitia muziki wake.

Hitmaker huyo wa “Bingi Bango” amewajibu wanaodai kuwa uhusiano wake na Pritty Vishy ni kiki kwa kusema kuwa hana muda wa kuwaaminisha watu kuwa anatoka kimapenzi  na mrembo huyo kwa kuwa masuala ya mahusiano ni ya watu wawili.

Mbali na hayo amezungumzia ishu ya kuwaachumbia wanawake walioachwa na mastaa wenzake kwa kusema kwamba wanawake sampuli hiyo ni wapambanaji lakini pia wanajua sana mapenzi ikilinganishwa na wanawake wa watu wasiokuwa na umaarufu.

Hata hivyo amewataka wakenya waache kumshambulia pamoja na mpenzi wake pritty vishy kwa kuwa penzi lao ni la kweli na hivi karibuni wana mpango wa kuhalalisha ndoa yao kwa njia ya harusi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke