Mkali wa muziki nchini Madini Classic amewashangaza wadau wa muziki nchini baada ya kutangaza kwamba amekukumbatia mapenzi ya jinsia moja kwani amechoshwa na mapenzi kabisa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost picha akiwa amejipodoa wanja, na lipstick kama mwanamke na kusema kwamba ameamua kuhamia mapenzi ya jinsia moja kwani siyo dhambi.
Hitmaker huyo wa Toto la Kanairo amewaomba mashabiki wake kutomchukulia vibaya kwani ameumizwa sana kwenye mahusiano yake ya zamani hadi amekata tamaa kuanza mahusiano na wanawake.
Hata hivyo mashabiki zake wameonekana kukerwa na kauli ya Madini Classic huku wengi wakimtaka atoe muziki mzuri badala ya kujihusisha na kiki zisizokuwa na msingi aachane na masuala ya kiki nmuziki kama ameshindwa kuipambania kazi