Msanii kutoka Mombasa Madini Classic amelazimika kumkingia kifua mpenzi wake mpya baada ya rafiki yake kudai kwamba ikiwa atamuoa Pritty, hatamzalia watoto wazuri.
Kupitia ukurasa wake wa instagram, Madini amesema kuwa mchumba wake Pritty si kama wanawake wengi kwa sababu huwa Hariri picha anazoziweka kwenye mitandao yake ya kijamii.
“Sielewi ni kwa nini wengi wenu mnafikiri Pritty si mrembo ni kwa sababu hachapishi picha zilizohaririwa mtandaoni kama baadhi yenu? Get to meet that chil physically utakubaliana nami that’s cute,” Madini aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Habari za wawili hao kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi zilianza kusambaa mapema mwezi uliopita, ambapo walikuja wakathibitisha kuwa ni wapenzi na hata wakaanza kusambaza picha zao wakiwa kwenye pozi za kimahaba zaidi kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii na blogu mbali mbali.