You are currently viewing MADINI CLASSIC KWENYE PENZI JIPYA NA BABY MAMA WA MULAMWAH,CAROL SONNIE

MADINI CLASSIC KWENYE PENZI JIPYA NA BABY MAMA WA MULAMWAH,CAROL SONNIE

Msanii wa muziki nchini Madini Classic amethibitisha kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Carol Sonnie ambaye ni Baby Mama wa mchekeshaji maarufu  Mulamwah.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram msanii huyo ameweka wazi taarifa hiyo kwa mashabiki zake baada ya kuposti picha ya pamoja na mrembo huyo wakiwa kwenye pozi la kimahaba zaidi huku akiambatanisha na maneno yanayosomeka “Call me Mr. Polygamous. Wife number 2.”, akiashiri kuwa mrembo huyo amekubali kuwa mke wake wa pili.

Ni kitendo ambacho kimeibua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambapo wengi wameonekana kumpongeza madini Classic kwa hatua ya kumpata mpenzi mpya huku wengine wakitilia shaka mahusiano yao kwa kusema kwamba huenda ni kiki ya kutangaza ngoma mpya ya Madini Classic.

Utakumbuka Carol Sonnie na Baby Daddy wake Mulamwah walitangaza kuvunja mahusiano yao mwishoni mwa mwaka wa 2021 baada ya kukaa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa takriban miaka 5.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke