You are currently viewing MADOCHO WA KANAIRO ALAMBA SHAVU YA UBALOZI NCIC

MADOCHO WA KANAIRO ALAMBA SHAVU YA UBALOZI NCIC

Msanii maarufu wa tattoo nchini Kenya Madocho wa Kanairo amelamba shavu la kuwa balozi wa Tume ya uwiano na utangamano NCIC.

Akizungumza baada ya kutangaza kuwa balozi wa tume hiyo, Madocho amewataka vijana kote nchini kujitenga na uhalifu pamoja na kueneza chuki mitandaoni kwa kutumia maneno ambayo hayawezi kuchochea na kuleta uhasama miongoni mwa wa kenya kipindi hiki cha kampeini za kisiasa.

Mwenyekiti wa tume hiyo Dr. Samuel Kobia amesema kuteuliwa kwa Madocho kutasaidia pakubwa kusambaza na kuhubiri amani kwa vijana hasa wakati huu taifa inapoelekea kwenye uchaguzi wa Agosti 9 mwaka huu.

Kuchaguliwa kwa Madocho kuwa balozi wa NCIC imekuja mara baada ya tume hiyo kupiga marufuku baadhi ya maneno kutumika kwenye majukwaa ya kisiasa kama njia ya kuzuia vurugu kipindi cha uchaguzi.

Maneno hayo ni kama Sipangwingwi, Kama ni noma noma, Kaffir, Chunga kura, uncircumcised, fumigation, eliminate, kill na nyingine nyingi.

Utakumbuka Madacho wa Kanairo alipata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii nchini alipokuja na maneno ya lugha ya Sheng yanayosomeka “Kama unajinauwo venye unajinauwo, monchoka ukuje ubanje hapa kwa ghetto tukuskizze”

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke