You are currently viewing MAGIX ENGA AELEZA JINSI UKOSEFU WA SUPPORT UMEATHIRI PAKUBWA TASNIA YA MUZIKI NCHINI KENYA

MAGIX ENGA AELEZA JINSI UKOSEFU WA SUPPORT UMEATHIRI PAKUBWA TASNIA YA MUZIKI NCHINI KENYA

Prodyuza na mwanamuziki Magix Enga ameibuka na kudai tasnia ya muziki nchini Kenya ni mbovu ikilinganishwa na mataifa mengine.

Kupitia instagram page yake Enga amesema kiwanda cha muziki nchini kinaangazia sana taarifa mbaya za wasanii badala ya kuwapa support wasaniii kwenye muziki wao ili waweze kuingiza kipato ambacho kitawainua kiuchumi.

Hitmaker huyo “Kale” amesema  wasanii wengi wakongwe wanaishi kwenye lindi la umaskini kutokana na kukosa mazingira mazuri ya kutumia sanaa yao kuboresha maisha yao.

Hata hivyo watumiaji wengi kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kumuunga mkono kwa kauli yake hiyo huku wakitoa shime kwa washikadau wa masuala ya sanaa nchini kutatua changamoto zinazowakwamisha wasanii kutopata pesa za kuwasaidia kimaisha kupitia kazi zao za muziki.

Utakumbukwa juzi kati Magix Enga alishika headlines za habari za burudani nchini baada ya kukiri hadharani kwamba stori yake ya kuwa muumini wa dhehebu la illuminati ilikuwa batili kitu kilichowakasirisha sana walimwengu kwenye mitandao ya kijamii.

 

 

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke