You are currently viewing MAGIX ENGA AKANUSHA KUWA MUUMINI WA ILLUMINATI, ADAI NI KIKI

MAGIX ENGA AKANUSHA KUWA MUUMINI WA ILLUMINATI, ADAI NI KIKI

Prodyuza na msanii muziki nchini Magix Enga ameibuka na kukanusha taarifa alizozitoa awali  akidai kuwa ni muumini wa dhehebu la illuminatti.

Akiwa kwenye moja ya interview Enga amesema hajawahi kuwa muumini wa illuminati na wala haaminii katika uwepo wa dhehebu hilo.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Kale” ametoa changamoto kwa vijana nchini kujituma katika maisha badala ya kutumia njia ya mkato kutafuta mali.

Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao wa kijamii wamekerwa na matamshi ya magix enga wengi wakihoji kuwa huenda prodyuza huyo amepokea vitisho kutoka kwa viongozi wa dhehebu la illuminati ndio maana amebadili kauli yake kuhusu dhehebu hilo.

Wameenda mbali na kumtaka Magix Enga atafute kitu kingine cha kufanya badala ya kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwa vitu ambavyo havina msingi kwani muziki umemshinda.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke