You are currently viewing MAGIX ENGA AKIRI KUWA MUUMINI WA DHEHEBU LA KISHETANI LA ILLUMINATI

MAGIX ENGA AKIRI KUWA MUUMINI WA DHEHEBU LA KISHETANI LA ILLUMINATI

Mtayarishaji wa muziki kutoka kenya Magix Enga amefunguka na kukiri kuhusu yale aliyopitia baada ya kujiunga na dini ya kishetani.

Kwenye mahojiano na Plug TV, Magix amekiri kwamba umaskini ulimshinikiza kukubali kujiunga na dhehebu hiyo baada ya mwanadada mmoja wa kizungu kujitolea kumsaidia kujipatia utajiri mkubwa kutokana na  taaluma yake.

“Kila mwezi nilikuwa napokea pesa. Kuna gari fulani ilikuwa inakuja kila mwezi naambiwa niingie. Nilikuwa nakalia kiti cha nyuma lakini sikuwa naangalia ni nani alikuwa anaendesha. Ningechukua pesa zangu kisha narudi studioni. Nilikuwa napata pesa  nyingi.” amesema Magix Enga

Mtayarishaji huyo ameweka wazi kwamba hakuna karatasi zozote ambazo alitia saini na hakuna mtu yeyote ambaye alitoa kafara ila walikuwa wakitoa damu yake kwa kumtoboa kwenye tumbo.

Licha ya manufaa yote ya kifedha ambayo alikuwa akiyapata Magix ameeleza kuwa alifikia uamuzi wa kuachana na dini hiyo ya kishetani baada ya kuanza kupatiwa maagizo ambayo hangeweza kutimiza huku akiweka wazi kwamba kwa sasa hayuko tena katika dhehebu hiyo na tayari amemkubali yesu na kuokoka licha ya kundelea kuwindwa na wanachama wa madhehebu ya illuminatti.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke