You are currently viewing Magix Enga aomba mashabiki msamaha kwa masaibu yanayomuandama maishani

Magix Enga aomba mashabiki msamaha kwa masaibu yanayomuandama maishani

Ni majuto tu upande wa prodyuza Magix Enga, mkali huyo wa midundo kutoka nchini Kenya amekiri kupitia nyakati ngumu sana kwenye maisha yake.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook anajutia ni kwanini amekuwa akitengeneza kiki zisizo kuwa na mashiko katika jamii ambapo ameenda mbali zaidi na kuwaomba mashabiki zake msamaha kwa sarakasi ambazo amekuwa akijihusisha nayo kwenye mitandao ya kijamii.

“Hey my people place life imenifikisha I don’t understand anything nawapenda sana. Talent Iko though siko poa. Am going through a lot sielewi mbona somebody please. Kama nilikosea I apologize. More love to all of you”, Aliandika.

Utakumbuka miezi kadhaa iliyopita video yake akiwa mlevi chakari ilisambaa sana mtandaoni ambapo watu wengi walihuzunishwa na hali yake wakitoa rai kwa wahisani kujitokeza na kumsaidia prodyuza huyo kutokana na uraibu wa pombe ulioathiri maisha.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke