Prodyuza wa muziki nchini Magix Enga ametangaza ujio wa EP yake mpya ambayo ana mpango wa kuachia ndani ya mwaka huu wa 2022.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Magix Enga amewataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kuipokea EP yake hiyo ambayo kwa mujibu wak ameipa jina la Mawazo EP.
Hata hivyo hajeweka wazi Idadi ya ngoma wala tarehe rasmi ambayo EP yenyewe itaingia sokoni ila ameachia nyimbo mbili kutoka kwenye EP ambazo ni Ma-Pressure na Nakuwaza.
Hii inaenda kuwa EP ya pili kwa mtu mzima Magix Enga tangu aanze safari yake ya muziki baada ya Reason EP iliyotoka mapema mwaka huu ikiwa na jumla ya nyimbo 5 za moto.