You are currently viewing MAHAKAMA YAAHIRISHA KESI ILIYOWASILISHWA NA RINGTONE DHIDI YA MWANABLOGU ROBERT ALAI

MAHAKAMA YAAHIRISHA KESI ILIYOWASILISHWA NA RINGTONE DHIDI YA MWANABLOGU ROBERT ALAI

Mahakama ya Kibera imeahirisha kwa mara nyingine kikao cha kusikiliza kesi iliyowasilishwa na mwanamuziki Ringtone dhidi ya mwanablogu Robert Alai ambaye alimshambulia na kumjeruhi vibaya mwaka wa 2021.

Akizungumza nje ya mahakama ya kibera Wakili wa Ringtone Evans Ondiek amesema Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 3 mwaka wa 2022,baada ya wakili wa Robert alai kukosa kufika mahakamani kusikiliza ushahidi ambao ringtone alipaswa kuwasilisha dhidi ya mteja wake.

Ondiek ambaye alifika mahakamani akiwa kwenye kiti cha magurudumu baada ya kupata ajali, amemlaumu wakili wa Robert alai kwa kuihadaa mahakama kila mara kuisukuma mbele kesi ya mteja wake huku akisema kuwa ana njama ya kusambaratisha kesi inayomkabili mshatakiwa.

Kwa upande Mwanamuziki Ringtone amesema atakata tamaa kwenye kesi dhidi ya Robert Alai hadi pale mahakama itamtendea haki ikizingatiwa kuwa ana ushahidi wa kutosha dhidi ya mwanablogu huyo ambaye alimjeruhi vibaya kichwani kwa rungu.

Hii ni  mara ya tatu kwa kesi hiyo kuaahirishwa, mapema mwezi Februari mwaka huu ilisogeza mbele hadi Mei 9 baada ya mahakama kushikika kwenye majukumu mengine.

Utakumbuka Ringtone na Robert Alai waliingia kwenye ugomvi mwezi julai mwaka wa 2021 baada ya wawili hao kuhusika kwenye ajali ya barabarani ambapo ringtone alimtuhumu Alai kwa kumpiga Rungu ya kichwa na kuaharibu gari lake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke