You are currently viewing MAHAKAMA YAMUAMURU DIANA MARUA KUFUTA VIDEO YA TUHUMA ZA UBAKAJI DHIDI YA WILLY PAUL

MAHAKAMA YAMUAMURU DIANA MARUA KUFUTA VIDEO YA TUHUMA ZA UBAKAJI DHIDI YA WILLY PAUL

Mahakama ya Milimani nchini Kenya imemuamuru Diana Marua kufuta video aliyotengeneza akidai kuwa mwanamuziki Willy Paul alijaribu kumbaka.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Willy Paul alichapisha picha ya karatasi ya amri za mahakama iliyotiwa saini na hakimu mkuu mwandamizi D.W Mburu.

Amri hiyo ya mahakama inamtaka Diana Marua kufuta video ambayo alipakia YouTube mnamo Desemba 9 ikielezwa kuwa madai yake yameathiri kazi na afya ya Willy Paul.

“Inaamriwa kuwa video ya mshtakiwa/mlalamikiwa na chapisho la mitandao ya kijamii lililochapishwa kwenye chaneli yake ya YouTube yenye jina la ‘My Untold Story, Willy Paul tried to rape me’, lfutwe ikusubiriwa kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi yake kwa vile linamuathiri mlalamishi, kumfanya apoteze fursa za biashara na kumfanya ateseke kiafya” Karatasi hiyo ilisomeka.

Mahakama pia imemtahadharisha Diana na washirika wake dhidi ya kumharibia jina Willy Paul ikisubiriwa kusikilizwa kwa kesi aliyowasilisha mahakamani. Onyo kali imetolewa kwa yeyote atakayekaidi amri hiyo ya mahakama ambayo ilitolewa tarehe 29 Desemba.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke