You are currently viewing MISS P AAGIZWA KUFUTA VIDEO YA SAKATA LA WILLY PAUL KUMYANYASA KIMAPENZI

MISS P AAGIZWA KUFUTA VIDEO YA SAKATA LA WILLY PAUL KUMYANYASA KIMAPENZI

Mahakama imemuagiza msanii Miss P kufuta video zote akimtuhumu Willy Paul kuwa alimdhulumu kimapenzi kwenye mtandao wa Youtube.

Kupitia nyaraka ambazo Willy Paul ameshare kwenye ukurasa wake wa Instagram mahakama imemtaka msanii huyo afute video hizo mara moja la sivyo atakabiliwa kisheria iwapo atakwenda kinyume na agizo la mahakama.

Ikumbukwe mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu Miss P alijitokeza kwa mara ya kwanza baada ya ukimya wa muda mrefu na kudai kwamba aliigura lebo ya Saldido kwa sababu Willy Paul alimnyanyasa kimapenzi. Jambo ambalo lilimfanya Willy Paul kufungua shauri mahakamani akidai kwamba Miss P alimuaharibi brand yake kwa kumzushia tuhuma za uongo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke