Staa wa muziki wa Bongo Fleva Malkia Karen amejibu kwa vitendo tetesi za kubeba ujauzito.
Karen ametumia ukurasa wake wa Instagram kupost video ambayo ni kionjo cha video ya wimbo wake mpya alioupa jina la Haina Haja huku akionekana kuwa ni mjamzito wa mimba kubwa.
Kwenye kionjo cha wimbo huo Malkia Karen anasikika akimlaumu mwanume ambaye alikuwa naye kwenye mahusiano lakini mwisho wa siku akaja kumtenda vibaya.
Tetesi za Malkia Kareen kubeba ujauzito zili trend sana kwenye mitandao ya kijamii wiki kadhaa zilizopita na ujauzito huo ulihusishwa kuwa ni wa staa wa muziki Diamond Platnumz japo hakuna yeyote kati ya wawili hao aliyejitokeza kuthibitisha taarifa hizo.