Baada ya Chrisean kudai kuwa ana ujauzito wa Blueface, mama mzazi wa rapa huyo ameibuka na kufunguka kuwa mrembo huyo hana ujauzito.
Mama mzazi wa Blueface anayefahamika kwa jina la Karlissa ametumia instastory yake kumchana mkwewe kuwa aache kucheza michezo ya kitoto kwani anajua fika kuwa hana ujauzito. Na katika kupigilia msumari ili swala hilo amemtaka Chrisean kufanya kipimo cha ujauzito Live instagram kama ni kweli ana ujauzito.