Mwanamama Kris Jenner amekanusha kuhusika kwenye biashara ya kusambaza mkanda wa ngono ambao ulimuhusisha binti yake Kim Kardashian na Ray J mwaka 2007.
Kris Jenner amekanusha tuhuma hizo ambazo zilitolewa na Ray J wiki hii ambaye alidai kwamba video ile ya ngono haikuvuja bali ilikuwa ni makubaliano ya Kibiashara baina yake, Kim Kardashian pamoja na Kris Jenner.
Utakumbuka kuwa Oktoba mwaka 2002 Kim Kardashian na Ray J walirekodi mkanda wa Ngono wakiwa mapumzikoni nchini Mexico.
Mwaka 2007 kampuni ya Vivid Entertainment iliripotiwa kununua haki za mkanda huo kwa $1 million na ndio ulikuwa mwanzo wa Kim Kardashian kupata umaarufu duniani kote.