You are currently viewing Mama mzazi wa msanii Trio Mio amkingia kifua kwa madai ya kufeli mtihani wa KCSE 2022

Mama mzazi wa msanii Trio Mio amkingia kifua kwa madai ya kufeli mtihani wa KCSE 2022

Mama mzazi wa msanii Trio Mio, Irma Sofia amepuzilia mbali madai yanayotembea mtandaoni kuwa mwanaye alipata alama ya D kwenye mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE.

Kupitia mitandao yake kijamii mwanamama huyo amemkingia kifua mwanaye kwa kusema kuwa hitmaker huyo wa “Cheza Kama Wewe” alifanya vizuri kwenye mtihani huo na anajivunia matokeo yake.

“Kooo Sasa Sitabreathe coz KCSE results zimetoka?? Tulieni. The boy did his best and am very proud of him. And those speculating a D ….poleni!”, Ujumbe wake ulisomeka.

Mara tu baada ya waziri wa elimu Ezekiel Machogu kutangaza rasmi matokeo hayo, walimwengu kwenye mitandao ya kijamii waliibua madai kuwa Trio Mio alipata alama ya D kwenye mtihani wa KCSE 2022.

Hata hivyo mpaka sasa hajabainika wazi msanii huyo amepata alama ipi kwenye wa ke wa KCSE ila baadhi ya wajuzi wa mambo mitandaoni wanadai kuwa alipata alama ya A-.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke