Klabu ya Manchester United imetangaza kumalizana na nyota wake Cristiano Ronaldo. Man United imetoa taarifa rasmi usiku huu kwamba, pande zote mbili zimefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na nyota huyo anatakiwa kuondoka haraka iwezekanavyo.
Ronaldo anaondoka Man United kufuatia mahojiano yake na Piers Morgan ambayo yaliishambulia Klabu pamoja na menejimenti. Kwenye tamko lake la mwisho, CR7 amesema anaipenda Man United na anawapenda mashabiki, ila ni muda wa kutafuta changamoto mpya.