You are currently viewing MAPANCH NA MARIOO WATUPIANA LAWAMA KUHUSU WIMBO WA “MY LOVE”

MAPANCH NA MARIOO WATUPIANA LAWAMA KUHUSU WIMBO WA “MY LOVE”

Agosti 10, msanii wa Bongfleva Mapanch aliachia video ya ngoma yake My Love aliyomshirikisha Marioo. Hata hivyo takriban siku nne baadaye, video hiyo iliondolewa youtube.

Mapanch anadai aliyeiondoa ni Marioo ambaye alituma malalamiko ya hakimiliki.

Msanii huyo amesema amechukizwa na kitendo hicho kwa kueleza kuwa Marioo ni mnafiki na mbaya zaidi ni yeye ndiye aliyetaka kuwepo kwenye wimbo huo.

Hata hivyo Marioo amezungumza kwanini hakutaka video ya My Love aliyoshirikishwa na mapanch itoke.

Marioo amesema ngoma hiyo ilikaa sana ndani licha ya kuwahimiza mara kadhaa wawaiache kuitoa kwa sababu muziki wake unabadilika kadri siku zinavyokwenda.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke