Watayarishaji wawili wa muziki kutoka nchini Tanzania Blacq Beatz na S2kizzy wameonekana kutofautiana katika mtazamo wa maprodyuza kutohusika katika mgao wa mirabaha ya muziki iliyotolewa usiku wa kuamkia Januari 29.
Hili limekuja baada ya Chama cha Hakimiliki Tanzania COSOTA kwa kushirikiana na wizara ya sanaa kutoa sehemu ya fedha zilizopatikana kwenye kazi za wanamuziki {mirabaha} huku watayarishaji wa muziki wa Bongofleva wakisahaulika kwenye orodha hiyo.
S2kizzy ameonekana kutofurahishwa na jambo hilo huku Blacq akijibu kuwa jambo hilo limetokana na wao kama maprodyuza kutojua thamani na haki yao, ambapo amesema maprodyuza wa Bongofleva waendelee kusubiri kusaidiwa na wasanii.