You are currently viewing MARAPA OCTOPIZZO NA KAYVO KFORCE WARUSHIANA MAKONDE KISA DISS-TRACK

MARAPA OCTOPIZZO NA KAYVO KFORCE WARUSHIANA MAKONDE KISA DISS-TRACK

Mastaa wa muziki wa Rap Nchini Octopizzo na Kayvo Kforce  karibu warushiane makonde baada kuingia kwenye mzozo mkali huko Jiji Nairobi.

Rappers hao ambao walikutana uso kwa uso kwenye podcast ya mwafrika iitwayo Iko Nini wameonekana katika video wakipiga kelele na kutukanana wakati wakizuiwa na Walinzi wao.

Ikumbukwe Octopizzo na Kayvo Kforce  wamekuwa katika bifu kwa wiki kadhaa sasa baada ya  Kayvo Kforce kuikosoa album mpya ya rapa Octopizzo iitwayo Fuego kwa kusema kwamba ni album mbovu kuachiwa mwaka huu.

Hata hivyo  jambo ambalo lilimfanya Octopizo kumkana Kayvo Kforce  kwenye moja ya interview kwa kusema kwamba rapa huyo sio mzaliwa wa Kibera kwani tangu wafahamiane hajawahi jua maeneo ambayo anatokea.

Baada ya wawili kurushiana maneno makali Kayvo Kforce  ameamua kuachia distrack iitwayo nyumba kumi ambayo amemvua nguo Octopizzo kwa kusema kwamba muziki wake umepoteza mvuto hivyo akome kutumia jina lake kujitafutia umaarufu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke